Exodus 15:6-11


6 a“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana
ulitukuka kwa uweza.
Mkono wako wa kuume, Ee Bwana,
ukamponda adui.
7 bKatika ukuu wa utukufu wako,
ukawaangusha chini wale waliokupinga.
Uliachia hasira yako kali,
ikawateketeza kama kapi.
8 cKwa pumzi ya pua zako
maji yalijilundika.
Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta,
vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

9 d“Adui alijivuna,
‘Nitawafuatia, nitawapata.
Nitagawanya nyara;
nitajishibisha kwa wao.
Nitafuta upanga wangu
na mkono wangu utawaangamiza.’
10 eLakini ulipuliza kwa pumzi yako,
bahari ikawafunika.
Wakazama kama risasi
kwenye maji makuu.

11 f“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana?
Ni nani kama Wewe:
uliyetukuka katika utakatifu,
utishaye katika utukufu,
ukitenda maajabu?
Copyright information for SwhNEN