d Kut 32:8; 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-23; 27:15; 2Sam 7:22; 1Fal 14:9; 2Fal 17:12; Isa 42:8; 44:9
eKut 23:13; Yos 23:7; Amu 6:10; 2Fal 17:35; Isa 44:15-19; 46:6; Kut 34:14; Kum 4:24; Yos 24:19; Mwa 9:25; Law 26:39; Kut 34:7; Hes 14:18; Yer 32:18
g Kut 22:28; Law 18:21; 19:12; 22:2; 24:11, 16; Kum 6:13; 10:20; Ay 2:5-9; Za 63:11; Isa 8:21; Eze 20:39; 39:7; Mt 5:33
l Kum 5:16; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2; Kum 6:2; Efe 6:3; Kum 11:9; 25:15; Yer 35:7
n Law 18:20; 20:10; Hes 5:12, 13, 29; Mit 6:29-32; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11
p Law 19:11; Yer 9:3-5; Kut 23:1, 7; Law 19:18; Za 50:20; 101:5; 119:29; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 3:14; 18:20
r Kut 19:16-19; Kum 4:36; Isa 58:1; Yer 6:17; Eze 33:3; Ebr 12:1-19; Ufu 1:10; Kut 19:18; Mwa 3:10; Kut 14:31; 19:16
Exodus 20:1-23
Amri Kumi
(Kumbukumbu 5:1-21)
1 aNdipo Mungu akasema maneno haya yote:2 b“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.
3 cUsiwe na miungu mingine ila mimi.
4 dUsijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 eUsivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 flakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
7 gUsilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
8 hIkumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9 iKwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10 jlakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 kKwa kuwa kwa siku sita, Bwana aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.
12 lWaheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.
13 mUsiue.
14 nUsizini.
15 oUsiibe.
16 pUsimshuhudie jirani yako uongo.
17 qUsiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”
Watu Wanaogopa
(Kumbukumbu 5:22-33)
18 rWatu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 19 sna wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”20 tMose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.”
21 uWatu wakabaki mbali, wakati Mose alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa.
Sanamu Na Madhabahu
22 vKisha Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni: 23 wMsijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.
Copyright information for
SwhNEN