Exodus 25:10-22
Sanduku La Agano
(Kutoka 37:1-9)
10 a“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, ▼▼Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5.
upana wa dhiraa moja na nusu, ▼▼Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.
na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11 dUtalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13 eKisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14 fUtaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15 gHiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. 16 hKisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa. 17 i“Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. 18 jTengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 19Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 20 kMakerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. 21 lWeka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. 22 mHapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.
Copyright information for
SwhNEN