Exodus 27:1-8
Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa
(Kutoka 38:1-7)
1 a“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; ▼▼Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.
itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, ▼▼Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.
na upana wake dhiraa tano. 2 dTengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. 3 eTengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. 4Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. 5Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 6 fTengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. 7 gHiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. 8 hTengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.
Copyright information for
SwhNEN