Exodus 29:38-41
38 a“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 39 bUtamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 40 cPamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja ▼▼Efa moja ni sawa na kilo 22.
ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini ▼▼Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. 41 fHuyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
Copyright information for
SwhNEN