Exodus 35:1-4
Masharti Ya Sabato
1 aMose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayo Bwana amewaamuru ninyi mfanye: 2 bKwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwa Bwana. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe. 3 cMsiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.”Vifaa Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu
(Kutoka 25:1-9)
4 dMose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Bwana aliloamuru:
Copyright information for
SwhNEN