Ezekiel 18:12-16

12 aHuwaonea maskini na wahitaji.
Hunyangʼanyana.
Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.
Huziinulia sanamu macho.
Hufanya mambo ya machukizo.
13 bHukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.
Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

14 c“Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:

15 d“Hakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima,
wala hainulii macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi
mke wa jirani yake.
16 eHakumwonea mtu yeyote
wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo.
Hanyangʼanyi,
bali huwapa wenye njaa chakula chake
na huwapa nguo walio uchi.
Copyright information for SwhNEN