Ezekiel 26:17-18
17 aNdipo wao watakuombolezea na kukuambia:“ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa,
ee mji uliokuwa na sifa,
wewe uliyekaliwa na mabaharia!
Ulikuwa na nguvu kwenye bahari,
wewe na watu wako;
wote walioishi huko,
uliwatia hofu kuu.
18 bSasa nchi za pwani zinatetemeka
katika siku ya anguko lako;
visiwa vilivyomo baharini
vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’
Copyright information for
SwhNEN