Ezekiel 27:32-36

32 aWatakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako,
watafanya maombolezo kukuhusu wakisema:
“Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro,
katika moyo wa bahari?”
33 bWakati bidhaa zako zilipotoka baharini,
ulitosheleza mataifa mengi;
kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako
ulitajirisha wafalme wa dunia.
34 cSasa umevunjavunjwa na bahari,
katika vilindi vya maji,
bidhaa zako na kundi lako lote
vimezama pamoja nawe.
35 dWote waishio katika nchi za pwani
wanakustaajabia;
wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu,
nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.
36 eWafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka;
umefikia mwisho wa kutisha
nawe hutakuwepo tena.’ ”
Copyright information for SwhNEN