Genesis 15:1-4

Agano La Mungu Na Abramu

1 aBaada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono:

“Usiogope, Abramu.
Mimi ni ngao yako,
na thawabu yako kubwa sana.”
2 bLakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 3 cAbramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”

4 dNdipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.”
Copyright information for SwhNEN