Genesis 17:17-19
17 aAbrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18 bAbrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”19 cNdipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. ▼
▼Isaki maana yake Kucheka.
Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
Copyright information for
SwhNEN