Genesis 17:17-24
17 aAbrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18 bAbrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”19 cNdipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. ▼
▼Isaki maana yake Kucheka.
Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. 20 eKwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 21 fLakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 22 gWakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu. 23 hSiku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 24 iAbrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa,
Copyright information for
SwhNEN