Genesis 27:27-29
27 aKwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema,“Aha, harufu ya mwanangu
ni kama harufu ya shamba
ambalo Bwana amelibariki.
28 bMungu na akupe umande kutoka mbinguni
na utajiri wa duniani:
wingi wa nafaka na divai mpya.
29 cMataifa na yakutumikie
na mataifa yakusujudie.
Uwe bwana juu ya ndugu zako,
na wana wa mama yako wakusujudie.
Walaaniwe wale wakulaanio,
nao wale wakubarikio wabarikiwe.”
Copyright information for
SwhNEN