Genesis 31:45-53

45 aHivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. 46 bAkawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. 47 cLabani akaliita Yegar-Sahadutha
Yegar-Sahadutha maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiaramu.
na Yakobo akaliita Galeedi.
Galeedi maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiebrania.


48 fLabani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. 49 gPia liliitwa Mispa,
Mispa maana yake Mnara wa ulinzi.
kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.
50 iKama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

51 jPia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi. 52 kLundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru. 53 lMungu wa Abrahamu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.”

Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaki.
Copyright information for SwhNEN