Genesis 35:16-18

Vifo Vya Raheli Na Isaki

16 aKisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 17 bAlipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 18 cHapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.
Benoni maana yake Mwana wa huzuni yangu.
Lakini babaye akamwita Benyamini.
Benyamini maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.


Copyright information for SwhNEN