Genesis 49:8-10


8 a“Yuda, ndugu zako watakusifu;
mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako;
wana wa baba yako watakusujudia.
9 bEe Yuda, wewe ni mwana simba;
unarudi toka mawindoni, mwanangu.
Kama simba hunyemelea na kulala chini,
kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?
10 cFimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda,
wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake,
hadi aje yeye ambaye milki ni yake,
ambaye utii wa mataifa ni wake.
Copyright information for SwhNEN