Habakkuk 1:6-10
6Nitawainua Wakaldayo,watu hao wakatili na wenye haraka,
ambao hupita dunia yote
kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe.
7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;
wenyewe ndio sheria yao,
na huinua heshima yao wenyewe.
8Farasi wao ni wepesi kuliko chui,
na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo.
Askari wapanda farasi wao huenda mbio;
waendesha farasi wao wanatoka mbali.
Wanaruka kasi kama tai ili kurarua;
9 awote wanakuja tayari kwa fujo.
Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele
kama upepo wa jangwani,
na kukusanya wafungwa
kama mchanga.
10 bWanawabeza wafalme,
na kuwadhihaki watawala.
Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma;
wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.
Copyright information for
SwhNEN