Isaiah 1:28-31

28 aLakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa,
nao wanaomwacha Bwana wataangamia.

29 b“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni
ambayo mlifurahia,
mtafadhaika kwa sababu ya bustani
mlizozichagua.
30 cMtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka,
kama bustani isiyokuwa na maji.
31 dMtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto,
na kazi yake kama cheche ya moto;
vyote vitaungua pamoja,
wala hakuna wa kuuzima huo moto.”
Copyright information for SwhNEN