Isaiah 1:7-9
7 aNchi yenu imekuwa ukiwa,
miji yenu imeteketezwa kwa moto;
nchi yenu imeachwa tupu na wageni
mbele ya macho yenu,
imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni.
8 bBinti Sayuni ameachwa kama kipenu
katika shamba la mizabibu,
kama kibanda katika shamba la matikitimaji,
kama mji uliohusuriwa.
9 cKama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ▼
▼Bwana Mwenye Nguvu Zote hapa ni Yehova Sabaoth, yaani Bwana wa Majeshi; pia Warumi 9:29 na Yakobo 5:4.
asingelituachia walionusurika,
tungelikuwa kama Sodoma,
tungelifanana na Gomora.
Copyright information for
SwhNEN