Isaiah 13:6-9


6 aOmbolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

7 cKwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 dHofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwaka kama moto.

9 eTazameni, siku ya Bwana inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
Copyright information for SwhNEN