Isaiah 13:9-13


9 aTazameni, siku ya Bwana inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
10 bNyota za mbinguni na makundi ya nyota
havitatoa mwanga wake.
Jua linalochomoza litatiwa giza
na mwezi hautatoa nuru yake.
11 cNitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake,
waovu kwa ajili ya dhambi zao.
Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi,
na nitakishusha kiburi cha watu wakatili.
12 dNitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi,
watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 eKwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke,
nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake
katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika siku ya hasira yake iwakayo.
Copyright information for SwhNEN