Isaiah 15:4-6
4 aHeshboni na Eleale wanalia,sauti zao zinasikika hadi Yahazi.
Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele,
nayo mioyo yao imezimia.
5 bMoyo wangu unamlilia Moabu;
wakimbizi wake wanakimbilia Soari,
hadi Eglath-Shelishiya.
Wanapanda njia ya kwenda Luhithi,
wanakwenda huku wanalia;
barabarani iendayo Horonaimu
wanaombolezea maangamizi yao.
6 cMaji ya Nimrimu yamekauka
na majani yamenyauka;
mimea imekauka wala hakuna
kitu chochote kibichi kilichobaki.
Copyright information for
SwhNEN