Isaiah 19:5-7


5 aMaji ya mito yatakauka,
chini ya mto kutakauka kwa jua.
6 bMifereji itanuka;
vijito vya Misri vitapungua
na kukauka.
Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7 cpia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,
pale mto unapomwaga maji baharini.
Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,
litapeperushwa na kutoweka kabisa.
Copyright information for SwhNEN