Isaiah 2:10-17


10 aIngieni kwenye miamba,
jificheni ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake!
11 bMacho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa
na kiburi cha wanadamu kitashushwa,
Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.

12 c Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba
kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi,
kwa wote wanaojikweza
(nao watanyenyekezwa),
13 dkwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana,
na mialoni yote ya Bashani,
14 ekwa milima yote mirefu
na vilima vyote vilivyoinuka,
15 fkwa kila mnara ulio mrefu sana
na kila ukuta wenye ngome,
16 gkwa kila meli ya biashara,
Au: ya Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 60:9.)

na kila chombo cha baharini cha fahari.
17 i jMajivuno ya mwanadamu yatashushwa,
na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,
Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
Copyright information for SwhNEN