Isaiah 2:19-21


19 aWatu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,
na kwenye mahandaki ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia.
20 bSiku ile, watu watawatupia
panya na popo
sanamu zao za fedha na za dhahabu,
walizozitengeneza ili waziabudu.
21 cWatakimbilia kwenye mapango miambani
na kwenye nyufa za miamba
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia.
Copyright information for SwhNEN