Isaiah 22:16-18

16 aUnafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa
kujikatia kaburi lako mwenyewe,
ukichonga kaburi lako mahali palipo juu,
na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba?

17 b“Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti,
na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.
18 cAtakuvingirisha uwe kama mpira
na kukutupa katika nchi kubwa.
Huko ndiko utakakofia,
na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia,
wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!
Copyright information for SwhNEN