Isaiah 23:1-6
Unabii Kuhusu Tiro
1 aNeno kuhusu Tiro:Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi!
Kwa kuwa Tiro imeangamizwa,
imeachwa bila nyumba wala bandari.
Kuanzia nchi ya Kitimu ▼
▼Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania.
neno limewajia.
2 cNyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani,
pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni,
ambao mabaharia wamewatajirisha.
3 dKwenye maji makuu
nafaka za Shihori zilikuja;
mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro,
naye akawa soko la mataifa.
4 eUaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari,
kwa kuwa bahari imesema:
“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa,
wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”
5 fHabari ifikapo Misri,
watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.
6 gVukeni mpaka Tarshishi,
ombolezeni, enyi watu wa kisiwani.
Copyright information for
SwhNEN