Isaiah 28:15-17
15 aNinyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,tumefanya mapatano na kuzimu.
Wakati pigo lifurikalo litakapopita,
haliwezi kutugusa sisi,
kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu
na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”
16 bKwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo:
“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,
jiwe lililojaribiwa,
jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.
Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.
17 cNitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia
na uadilifu kuwa timazi;
mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,
nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.
Copyright information for
SwhNEN