Isaiah 40:18-20


18 aBasi, utamlinganisha Mungu na nani?
Utamlinganisha na kitu gani?
19 bKwa habari ya sanamu, fundi huisubu,
naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu
na kuitengenezea mikufu ya fedha.
20 cMtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii
huuchagua mti usiooza.
Humtafuta fundi stadi
wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.
Copyright information for SwhNEN