Isaiah 5:26-30


26 aYeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali,
anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia.
Tazama wamekuja,
kwa kasi na kwa haraka!
27 bHakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa,
hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala,
hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni,
hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika.
28 cMishale yao ni mikali,
pinde zao zote zimevutwa,
kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume,
magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.
29 dNgurumo yao ni kama ile ya simba,
wananguruma kama wana simba,
wanakoroma wanapokamata mawindo yao,
na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.
30 eKatika siku ile watanguruma juu yake
kama ngurumo za bahari.
Kama mtu akiitazama nchi,
ataona giza na dhiki;
hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.
Copyright information for SwhNEN