Isaiah 51:12-13


12 a“Mimi, naam mimi,
ndimi niwafarijie ninyi.
Ninyi ni nani hata kuwaogopa
wanadamu wanaokufa,
wanadamu ambao ni majani tu,
13 bkwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu,
aliyezitanda mbingu
na kuiweka misingi ya dunia,
kwamba mnaishi katika hofu siku zote
kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,
ambaye nia yake ni kuangamiza?
Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?
Copyright information for SwhNEN