Isaiah 55:3-5
3 aTegeni sikio mje kwangu,nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.
Nitafanya agano la milele nanyi,
pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.
4 bTazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa,
kiongozi na jemadari wa mataifa.
5Hakika utaita mataifa usiyoyajua,
nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia,
kwa sababu ya Bwana Mungu wako,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,
kwa maana amekutukuza.”
Copyright information for
SwhNEN