Isaiah 57:3-9


3 a“Lakini ninyi:
Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,
ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!
4 bMnamdhihaki nani?
Ni nani mnayemcheka kwa dharau,
na kumtolea ndimi zenu?
Je, ninyi si watoto wa waasi,
uzao wa waongo?
5 cMnawaka tamaa katikati ya mialoni
na chini ya kila mti uliotanda matawi;
mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde
na chini ya majabali yenye mianya.

6 d“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;
hizo ndizo sehemu yenu.
Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,
na kutoa sadaka za nafaka.
Katika haya yote,
niendelee kuona huruma?
7 eUmeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka,
huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.
8 fNyuma ya milango yako na miimo yako
umeweka alama zako za kipagani.
Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako,
umepanda juu yake na kukipanua sana;
ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao,
nawe uliangalia uchi wao.
9 gUlikwenda kwa Moleki
Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu.
ukiwa na mafuta ya zeituni,
na ukaongeza manukato yako.
Ukawatuma wajumbe wako mbali sana,
ukashuka kwenye kaburi
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
lenyewe!
Copyright information for SwhNEN