Isaiah 58:1-2
Mfungo Wa Kweli
1 a“Piga kelele, usizuie.Paza sauti yako kama tarumbeta.
Watangazieni watu wangu uasi wao,
na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao.
2 bKwa maana kila siku hunitafuta,
wanaonekana kutaka kujua njia zangu,
kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa,
na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake.
Hutaka kwangu maamuzi ya haki,
nao hutamani Mungu awakaribie.
Copyright information for
SwhNEN