Isaiah 59:16-18
16 aAliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja,akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati;
hivyo mkono wake mwenyewe
ndio uliomfanyia wokovu,
nayo haki yake mwenyewe
ndiyo iliyomtegemeza.
17 bAlivaa haki kama dirii kifuani mwake,
na chapeo ya wokovu kichwani mwake,
alivaa mavazi ya kisasi
naye akajifunga wivu kama joho.
18 cKulingana na kile walichokuwa wametenda,
ndivyo atakavyolipa
ghadhabu kwa watesi wake
na kisasi kwa adui zake,
atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.
Copyright information for
SwhNEN