Isaiah 63:2-6


2 aKwa nini mavazi yako ni mekundu,
kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

3 b“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;
kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.
Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu
na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;
damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,
na kutia madoa nguo zangu zote.
4 cKwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,
mwaka wa ukombozi wangu umefika.
5 dNilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,
nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;
hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,
na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
6 eNilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,
katika ghadhabu yangu niliwalewesha,
na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”
Copyright information for SwhNEN