Isaiah 65:6-7


6 a“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:
sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;
nitalipiza mapajani mwao:
7 bdhambi zenu na dhambi za baba zenu,”
asema Bwana.
“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima
na kunichokoza mimi juu ya vilima,
nitawapimia mapajani mwao
malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
Copyright information for SwhNEN