Isaiah 8:16-20


16 aFunga ushuhuda na kutia muhuri sheria
miongoni mwa wanafunzi wangu.
17 bNitamngojea Bwana,
ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.
Nitaliweka tumaini langu kwake.
18 cNiko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

19 dWakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunongʼona na kunungʼunika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 20 eKwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.
Copyright information for SwhNEN