‏ Jeremiah 11:13-17

13 aMnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’

14 b“Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao.

15 c“Mpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,
anapofanya mashauri yake maovu na wengi?
Je, nyama iliyowekwa wakfu yaweza
kuondolea mbali adhabu yako?
Unapojiingiza katika ubaya wako,
ndipo unashangilia.”

16 d Bwana alikuita mti wa mzeituni uliostawi
ulio na matunda mazuri kwa sura.
Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuu
atautia moto,
nayo matawi yake yatavunjika.
17 e Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.

Copyright information for SwhNEN