Jeremiah 22:10-16
10 aUsimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.
11 bKwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu ▼
▼Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi.
mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 12 dAtafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” 13 e“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,
vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,
akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,
bila kuwalipa kwa utumishi wao.
14 fAsema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,
na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’
Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,
huweka kuta za mbao za mierezi,
na kuipamba kwa rangi nyekundu.
15 g“Je, inakufanya kuwa mfalme
huko kuongeza idadi ya mierezi?
Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?
Alifanya yaliyo sawa na haki,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
16 hAliwatetea maskini na wahitaji,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”
asema Bwana.
Copyright information for
SwhNEN