Jeremiah 23:14-15
14 aNako miongoni mwa manabii wa Yerusalemunimeona jambo baya sana:
Wanafanya uzinzi
na kuenenda katika uongo.
Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,
kwa ajili hiyo hakuna yeyote
anayeachana na uovu wake.
Wote wako kama Sodoma kwangu;
watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”
15 bKwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:
“Nitawafanya wale chakula kichungu
na kunywa maji yaliyotiwa sumu,
kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu
kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.”
Copyright information for
SwhNEN