Jeremiah 25:15-26

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu

15 aHili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao. 16 bWatakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”

17 cHivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: 18 dYaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; 19 epia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote, 20 fpia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi); 21 gEdomu, Moabu na Amoni; 22 hwafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari; 23 iDedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali; 24 jwafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa; 25 kwafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi; 26 lna wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki
Sheshaki ni Babeli kwa fumbo.
atakunywa pia.

Copyright information for SwhNEN