Jeremiah 46:20-24


20 a“Misri ni mtamba mzuri,
lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.
21 bAskari wake waliokodiwa katika safu zake
wako kama ndama walionenepeshwa.
Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,
hawataweza kuhimili vita,
kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,
wakati wao wa kuadhibiwa.
22 cMisri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia
kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,
watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,
kama watu wakatao miti.
23 dWataufyeka msitu wake,”
asema Bwana,
“hata kama umesongamana kiasi gani.
Ni wengi kuliko nzige,
hawawezi kuhesabika.
24 eBinti wa Misri ataaibishwa,
atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”
Copyright information for SwhNEN