Jeremiah 49:1-3
Ujumbe Kuhusu Amoni
1 aKuhusu Waamoni:Hili ndilo asemalo Bwana:
“Je, Israeli hana wana?
Je, hana warithi?
Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?
Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake?
2 bLakini siku zinakuja,”
asema Bwana,
“nitakapopiga kelele ya vita
dhidi ya Raba mji wa Waamoni;
utakuwa kilima cha magofu,
navyo vijiji vinavyouzunguka
vitateketezwa kwa moto.
Kisha Israeli atawafukuza
wale waliomfukuza,”
asema Bwana.
3 c“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!
Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!
Vaeni nguo za gunia na kuomboleza,
kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,
kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni,
yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.
Copyright information for
SwhNEN