Jeremiah 49:13-17

13 aNinaapa kwa nafsi yangu,” asema Bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”

14Nimesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:
Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,
“Jikusanyeni ili kuushambulia!
Inukeni kwa ajili ya vita!”

15“Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,
aliyedharauliwa miongoni mwa watu.
16 bVitisho vyako na kiburi cha moyo wako
vimekudanganya,
wewe unayeishi katika majabali ya miamba,
wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.
Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,
nitakushusha chini kutoka huko,”
asema Bwana.
17 c“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;
wote wapitao karibu
watashangaa na kuzomea
kwa sababu ya majeraha yake yote.
Copyright information for SwhNEN