Jeremiah 49:7-22

Ujumbe Kuhusu Edomu

7 aKuhusu Edomu:

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Je, hakuna tena hekima katika Temani?
Je, shauri limewapotea wenye busara?
Je, hekima yao imechakaa?
8 bGeuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,
wewe uishiye Dedani,
kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau
wakati nitakapomwadhibu.
9Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,
wasingebakiza zabibu chache?
Kama wezi wangekujia usiku,
je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?
10 cLakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,
nitayafunua maficho yake,
ili asiweze kujificha.
Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,
naye hatakuwepo tena.
11 dWaache yatima wako; nitayalinda maisha yao.
Wajane wako pia
wanaweza kunitumaini mimi.”
12 eHili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. 13 fNinaapa kwa nafsi yangu,” asema Bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”

14Nimesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:
Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,
“Jikusanyeni ili kuushambulia!
Inukeni kwa ajili ya vita!”

15“Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,
aliyedharauliwa miongoni mwa watu.
16 gVitisho vyako na kiburi cha moyo wako
vimekudanganya,
wewe unayeishi katika majabali ya miamba,
wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.
Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,
nitakushusha chini kutoka huko,”
asema Bwana.
17 h“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;
wote wapitao karibu
watashangaa na kuzomea
kwa sababu ya majeraha yake yote.
18 iKama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,
pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”
asema Bwana,
“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.
Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.

19 j“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani
kuja kwenye nchi ya malisho mengi,
ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.
Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?
Ni nani aliye kama mimi,
na ni nani awezaye kunipinga?
Tena ni mchungaji yupi awezaye
kusimama kinyume nami?”
20 kKwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Edomu,
kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:
Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;
yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
21 lKwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.
Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.
Kwa Kiebrania ni Bahari ya Mafunjo.

22 nTazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,
akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.
Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu
itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Copyright information for SwhNEN