Jeremiah 50:30-32
30 aKwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;askari wake wote watanyamazishwa siku ile,”
asema Bwana.
31 b“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“kwa kuwa siku yako imewadia,
yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.
32 cMwenye majivuno atajikwaa na kuanguka,
wala hakuna yeyote atakayemuinua;
nitawasha moto katika miji yake,
utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
Copyright information for
SwhNEN