Jeremiah 50:41-43
41 a“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini;
taifa kubwa na wafalme wengi
wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.
42 bWamejifunga pinde na mikuki;
ni wakatili na wasio na huruma.
Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma
wanapoendesha farasi zao;
wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita
ili kukushambulia, ee Binti Babeli.
43 cMfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu,
nayo mikono yake imelegea.
Uchungu umemshika,
maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Copyright information for
SwhNEN