Jeremiah 51:37-43
37 aBabeli utakuwa lundo la magofuna makao ya mbweha,
kitu cha kutisha na kudharauliwa,
mahali asipoishi mtu.
38Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo,
wanakoroma kama wana simba.
39 bLakini wakati wakiwa wameamshwa,
nitawaandalia karamu
na kuwafanya walewe,
ili wapige kelele kwa kicheko,
kisha walale milele na wasiamke,”
asema Bwana.
40“Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni,
kama kondoo dume na mbuzi.
41 c“Tazama jinsi Sheshaki ▼
▼Sheshaki ni Babeli kwa fumbo.
atakamatwa,majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa.
Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani
kati ya mataifa!
42 eBahari itainuka juu ya Babeli;
mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika.
43 fMiji yake itakuwa ukiwa,
kame na jangwa,
nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake,
ambayo hakuna mtu anayepita humo.
Copyright information for
SwhNEN