Job 38:8-16
8 a“Ni nani aliyeifungia bahari milango
ilipopasuka kutoka tumbo,
9 bnilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,
na kuyafungia katika giza nene,
10 cnilipoamuru mipaka yake,
na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,
11 dniliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;
hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?
12 e“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,
au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,
13yapate kushika miisho ya dunia,
na kuwakungʼuta waovu waliomo?
14 fDunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;
sura yake hukaa kama ile ya vazi.
15 gWaovu huzuiliwa nuru yao,
nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.
16 h“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?
Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?
Copyright information for
SwhNEN